TUNAIMARISHA MIFUMO ITAKAYOZUIA WANYAMAPORI KUINGIA KATIKA MAKAZI YA WANANCHI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa sasa inaimarisha mifumo itakayozuia wanyamapori wakiwemo tembo kuingia katika makazi ya wananchi ili waweze kuishi kwa amani. Amesema baada ya Serikali kuimarisha ulinzi na kuzuia uwindaji haramu kwa sasa nchini kuna ongezeko kubwa la wanyama, hivyo inafanya jitihada kuzuia wanyama hao kuingia katika makazi. Ameyasema hayo leo (Alhamisi,